RAFIKI WA MAZINGIRA
Kwa Habari Picha na Ushauri tuandikie: Nature Friends Tanzania (NAFTA) Email: amtweveone@gmail.com, naturefriends@yahoo.com Mobile: +255754365850,+255754767594
Sunday, July 27, 2014
Thursday, January 17, 2013
Mfano wa fomu maalumu ya kuomba kuvuna mazao ya misitu Tanzania
Fomu hii imegawanyika katika sehemu A,B,C & D kama ifuatavyo:
SEHEMU A:Sehemu hii inatakiwa ijazwe na serikali ya kijiji/afisa mtendaji wa kijiji ambayo itaambatanishwa na muhtasari wa kikao cha serikali ya kijiji kilichokutana na kujadili maombi ya kampuni/mteja husika. Sehemu hii pia itaonyesha yafuatayo:
- Jina la kijiji na eneo la uvunaji……………………………..
- Jina la kampuni/mteja anayetaka kuvuna…………………..
- Aina,idadi na ujazo wa miti iliyokubaliwa………………….
- Aina na idadi ya miti anayotaka kuvuna…………………
- Jina na cheo (Mwenyekiti/Afisa Mtendaji) wa serikali ya kijiji………………………………………………………
- Sahihi ya mhuri wa kijiji……………………………………
SEHEMU B:Sehemu hii itajazwa na bwana miti wa sehemu/eneo uvunaji utakapofanyika.
Mambo muhimu ya kuzingatia:
- Jina la kijiji/kitongoji miti ilipo……………………………
- Jina la kampuni/mteja anayetaka kuvuna………………….
- Leseni ya biashara ya kampuni/mteja anayehusika………..
- Namba ya hati ya usajili wa kufanya biashara ya mazao ya misitu……………………………………………………….
- Aina ,idadi ya ujazo wa miti anayotaka kuvuna……………..
- Vipimo vya ujazo wa miti/magogo kama yalivyochukuliwa na bwana miti. Vipimo hivyo vitatajwa kwenye fomu maalumu (tree statement/log statement form)
- Jina la bwana mkiti na cheo chake…………………………
Sehemu hii itajazwa na afisa misitu wilaya baada ya kupata kibali cha kamati ya usimamizi wa uvunaji wa wilaya husika ambayo mwenyekiti wake ni mkuu wa wilaya baada ya mfanyabiashara wa mazao ya misitu kuwasilisha maombi (FDI) na atajibiwa kwa kukubaliwa/kukataliwa kwa fomu (FD2). Katika sehemu hii yafuatayo yatazingatiwa:
- Jina la afisa misitu wilaya husika…………………………
- Tarehe ya kikao na wajumbe waliohudhuria kujadili maombi hayo……………………………………………….
- Jina la kampuni/mteja aliyeruhusiwa……………………..
- Aina/idadi na ujazo wa miti/magogo yaliyoruhusiwa………
- Eneo miti/magogo yatakapovunwa…………………………
- Sahihi na mhuri wa afisa misitu wilaya husika…………….
Siku na muda wa upatikanaji wa hudumaIdara ya misitu na nyuki Tanzania inatoa huduma zake katika ofisi zake popote zilipo nchini siku zote za kazi (jumatatu – ijumaa) isipokua siku za jumamosi, jumapili au siku za sikukuu. Muda ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 alasiri.
Zingatia kwamba uvunaji wa mazao ya misitu nchini utasimamiwa na kamati za wilaya za usimamizi wa uvunaji misitu ambazo zitakuwa chini ya mkuu wa wilaya kama mwenyekiti. Mazao hayo ni yale tu yatakayovunwa kwa ajili ya biashara.
Tuesday, October 25, 2011
Tuesday, June 14, 2011
RISALA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI TAREHE MOSI APRILI 2011
.
Ndugu Wananchi,
Kama tunavyofahamu Tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti yalifanyika kwa mara ya kwanza tarehe Mosi Januari mwaka 2001 kutokana na Waraka wa Waziri Mkuu Namba 1 wa mwaka 2000 uliomtaka kila mwananchi kupanda miti kwa manufaa yake.
Kutokana na kiwango cha uponaji wa miti iliyopandwa kuwa kidogo, yaani kati ya asilimia 50 na 60 hasa kwenye maeneo kame kinachosababishwa na kupungua kwa mvua na athari za tabianchi, Waziri Mkuu alitoa Waraka mwingine Namba 1 wa Mwaka 2009, uliobadilisha Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka badala ya Januari Mosi. Mwezi Aprili ni mwezi ambao sehemu nyingi nchini zinapata mvua, hivyo ni wakati muafaka wa upandaji miti.
Mwaka jana Siku ya Taifa ya Kupanda Miti iliadhimishwa kitaifa Aprili Mosi kwa mara ya kwanza mkoani Shinyanga. Mwaka huu maadhimisho haya yatafanyika katika ngazi za mikoa yote nchini.
Kiutaratibu tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji pamoja na kupanda miti michache kama sehemu husika haitakuwa na mvua za kutosha. Kama kawaida, kila Mkoa umepanga siku maalum ya kupanda miti mingi zaidi kufuatana na majira ya mvua kwenye Mkoa husika.
Kwa mfano, Mkoa wa Pwani umepanga kupanda miti tarehe 15 Aprili, 2011. Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu watajiunga na wananchi wa Mkoa huo wakati watakapokuwa wanapanda miti katika msitu wa Kazimzumbwi Wilayani Kisarawe.
Ndugu wananchi
Maadhimisho ya mwaka huu ni ya pekee kwa maana ni mwaka ambao umetangazwa na Umoja wa Mataifa kama Mwaka wa Kimataifa wa Misitu. Ni mwaka wa kutafakari mchango wa watu wa mataifa yote katika kuilinda misitu na kuitumia kiuendelevu. Ni mwaka wa kuhamasishana kuendeleza uhifadhi na kupanda miti ili misitu iwanufaishe watu wa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Kwa hiyo, mwaka huu tutaitumia tarehe Mosi Aprili kuadhimisha Siku ya Taifa ya Kupanda Miti, pamoja na Mwaka wa Kimataifa wa Misitu.
Tukumbuke pia kuwa huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hivyo, tutaadhimisha siku hii kwa kutathmini tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kuhusiana na hali ya misitu. Kila mmoja wetu anatakiwa atathmini athari anazopata kutokana na ufyekaji na uharibifu wa misitu na kuamua kwa dhati kuhifadhi misitu, miti iliyopo nje ya misitu na kuongeza jitihada za kupanda kwa wingi miti ya asili na ya kigeni.
Ndugu Wananchi,
Sera ya Taifa ya Misitu imeweka umuhimu mkubwa katika kuhifadhi na kulinda misitu. Sera hii inahimiza ushiriki wa wananchi na wadau wengine kuihifadhi misitu iliyopo na kupanda miti na kuitunza.
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wananchi ambao wanastawisha miche ya miti bila kutegemea ile inayostawishwa katika bustani za serikali. Kwa sasa asilimia 70 ya miche ya miti yote inayopandwa inatokana na juhudi za wananchi wenyewe wanaoanzisha bustani ndogo zinazomilikiwa na vikundi vya kinamama, vijana, asasi zisizo za serikali, shule, na watu binafsi.
Ili kufanikisha upandaji miti nchini napenda kutumia fursa hii kutoa wito kuwa kila familia ianzishe bustani ndogo yenye miche angalau inayolingana na idadi ya wanafamilia. Kwa kufanya hivyo, ni rahisi kuitunza miche hiyo kwa kutumia maji yanayotumika nyumbani. Pale inapowezekana, ni vema familia zianzishe bustani kubwa kwa ajili ya biashara hivyo kuwawezesha wananchi wengi kupanda miti.
Wakati mwingine siyo lazima miche yote inayopandwa itoke bustanini. Njia nyingine ya kustawisha miti ni kutumia miche inayojiotea yenyewe ardhini kama maotea. Miche hiyo inapandwa katika sehemu zilizokusudiwa ikiwa bado midogo. Njia hii inatumika hasa kwenye sehemu zenye mvua nyingi na udongo tifutifu.
Njia nyingine ya kuongeza kiwango cha upandaji miti ni kupanda mbegu moja kwa moja ardhini kwa baadhi ya miti. Njia hii inatumika sana katika mikoa iliyoko katika nyanda za juu hapa nchini. Kwa mfano wakulima wa miwati katika mikoa ya Tanga na Iringa wanapanda mbegu moja kwa moja ardhini. Aidha, mikaratusi pia inaweza kupandwa kwa njia hii.
Aina nyingine ya kustawisha misitu ni kutenga na kulinda eneo kutokana na uharibifu wa kimazingira ili mbegu ziote zenyewe (yaani natural regeneration). Njia hii imefanikisha shughuli za kustawisha misitu na malisho ya mifugo mkoani Shinyanga. Wananchi wa Shinyanga wanatumia utaalam wao wa jadi unaojulikana kwa jina la Ngitili wa kutenga maeneo na kuyapumzisha ili mbegu zijiotee zenyewe. Matokeo yake ni eneo husika kubadilika na kuwa msitu.
Ustawishaji misitu kwa kutumia njia ya Ngitili umewawezesha wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuongoa zaidi ya hekta 500,000 za ardhi ambayo ilikuwa imeharibika kabisa hapo awali. Kutokana na uzoefu huo, nawaasa wananchi kutumia njia zao za jadi za kustawisha misitu na miti kwenye maeneo yao.
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwakumbusha na kuwahimiza kuwa kila mmoja wetu aitunze miti atakayoipanda kwa kuilinda dhidi ya uharibifu wa aina yoyote. Aidha, napenda kuchukua fursa hii kumhimiza kila mwananchi ajenge utamaduni wa kuitumia rasilimali ya misitu kwa njia endelevu kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria za kuvuna mazao mbalimbali ya misitu.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
RISALA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KATIKA KUADHIMISHA
SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI TAREHE MOSI APRILI 2011

Ndugu Wananchi
Baada ya kusema hayo, nawatakia wananchi wote maadhimisho mema ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti mwaka 2011.MISITU NI UHAI. PANDA MITI KWANZA NDIPO UKATE MTI
Mhe. Ezekiel M Maige.
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALI
Thursday, June 9, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)