Thursday, January 17, 2013

Mfano wa fomu maalumu ya kuomba kuvuna mazao ya misitu Tanzania

Fomu hii imegawanyika katika sehemu A,B,C & D kama ifuatavyo:
 
SEHEMU A:Sehemu hii inatakiwa ijazwe na serikali ya kijiji/afisa mtendaji wa kijiji ambayo itaambatanishwa na muhtasari wa kikao cha serikali ya kijiji kilichokutana na kujadili maombi ya kampuni/mteja husika. Sehemu hii pia itaonyesha yafuatayo:
  1. Jina la kijiji na eneo la uvunaji……………………………..
  2. Jina la kampuni/mteja anayetaka kuvuna…………………..
  3. Aina,idadi na ujazo wa miti iliyokubaliwa………………….
  4. Aina na idadi ya miti anayotaka kuvuna…………………
  5. Jina na cheo (Mwenyekiti/Afisa Mtendaji) wa serikali ya kijiji………………………………………………………
  6. Sahihi ya mhuri wa kijiji……………………………………

 SEHEMU B:Sehemu hii itajazwa na bwana miti wa sehemu/eneo uvunaji utakapofanyika.

Mambo muhimu ya kuzingatia:
  1. Jina la kijiji/kitongoji miti ilipo……………………………
  2. Jina la kampuni/mteja anayetaka kuvuna………………….
  3. Leseni ya biashara ya kampuni/mteja anayehusika………..
  4. Namba ya hati ya usajili wa kufanya biashara ya mazao ya misitu……………………………………………………….
  5. Aina ,idadi ya ujazo wa miti anayotaka kuvuna……………..
  6. Vipimo vya ujazo wa miti/magogo kama yalivyochukuliwa na bwana miti. Vipimo hivyo vitatajwa kwenye fomu maalumu (tree statement/log statement form)
  7. Jina la bwana mkiti na cheo chake…………………………
SEHEMU C:
Sehemu hii itajazwa na afisa misitu wilaya baada ya kupata kibali cha kamati ya usimamizi wa uvunaji wa wilaya husika ambayo mwenyekiti wake ni mkuu wa wilaya baada ya mfanyabiashara wa mazao ya misitu kuwasilisha maombi (FDI) na atajibiwa kwa kukubaliwa/kukataliwa kwa fomu (FD2). Katika sehemu hii yafuatayo yatazingatiwa:
  1. Jina la afisa misitu wilaya husika…………………………
  2. Tarehe ya kikao na wajumbe waliohudhuria kujadili maombi hayo……………………………………………….
  3. Jina la kampuni/mteja aliyeruhusiwa……………………..
  4. Aina/idadi na ujazo wa miti/magogo yaliyoruhusiwa………
  5. Eneo miti/magogo yatakapovunwa…………………………
  6. Sahihi na mhuri wa afisa misitu wilaya husika…………….
 SEHEMU D:Sehemu hii hutumika kwa maeneo ambayo uvunaji unasimamiwa na ofisi za hifadhi misitu za wilaya ambazo zimeteuliwa na idara.Vipengele vyake ni kama ilivyo sehemu “C” hapo juu.
 Siku na muda wa upatikanaji wa hudumaIdara ya misitu na nyuki Tanzania inatoa huduma zake katika ofisi zake popote zilipo nchini siku zote za kazi (jumatatu – ijumaa) isipokua siku za jumamosi, jumapili au siku za sikukuu. Muda ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 alasiri.
 
Zingatia kwamba uvunaji wa mazao ya misitu nchini utasimamiwa na kamati za wilaya za usimamizi wa uvunaji misitu ambazo zitakuwa chini ya mkuu wa wilaya kama mwenyekiti. Mazao hayo ni yale tu yatakayovunwa kwa ajili ya biashara.






No comments:

Post a Comment